Calling Lyrics by Professor Jay Ft Ali Kiba
Professor Jay Lyrics
Read and sing aloud Calling Lyrics by Professor Jay Ft Ali Kiba. The song has been well-received by fans in Tanzania.
Calling Lyrics by Professor Jay Ft Ali Kiba
Mmmh!!
Yeap!!!
Yeah
Professor j foundation
Bin laden
Amekuwa mkiwa, amegunikwa na unyonge
mwenye ukiwa wa njiwa, koo limekabwa na donge
Alikuwa na furaa, mama yake alipokuwepo
Gafla mama akazima kama ushumaa kwenye upepo
Kwenye umri mdogo hakuona pengo lolote
Zaidi ya kuchezacheza, bila ya kujua chochote
Adhabu ilianza alipokuja mama wa Kambo
mateso na maneno kila alipofanya jambo
Yeye alibaguliwa, hakupendwa kama wengine
alipewa kazi ngumu sana utadhani mashine
kutwa anashunda Njaa, moyon Hana furaa
ukimwangalia usoni amefubaa, ameshakata tamaa
haoni Tena sababu ya kuishi na ndugu zake
kutwa Yuko peke yake, akimlilia mama ake
Hana kosa lolote huyu malaika wa mungu
Hajatenda jambo baya, mnamwamuru atubu
She is calling ooh calling
Kwa waliopitia shida aaah,
kwani haya maisha, ipo siku yataisha
ipo na
usikate tamaa aaah, kwani hata mbuyuu ulianza kama mchichaa
jikaze tutafika, she is calling
Alipenda kusoma elimu ije kumsaidia
tabu alizozipata aliona azivumilie aliupenda urubani
ila elimu ikawa ndoto, shuleni kama vitani yaani amani amani ndani ya moto
akienda shuleni wenzake wanamcheka
nguo zimechakaa nafsi yake inakereka
alikuwa kama mtumishi asiyelipwa Mshahara
ilibidi afanye kazi aweze kulala
alipewa kazi ngumu tofaut na umri wake
ilibidi aongeze juhudi Ili aokoe nafsi yake
akifanya kosa dogo mikono inachomwa moto
hakika walimkomaza ilihali umri Bado mdogo
alimwomba mola wake ampunguzie mateso
Ili siku ipite walau waione kesho, mara nyingi alitoroka na kukimbilia mtaan
jua lake mvua yake analala barabarani
She is calling ooh calling
Kwa waliopitia shida aaah
kwani haya maisha, ipo siku yataisha
isha na
usikate tamaa aaah, kwani hata mbuyuu ulianza kama mchichaa
jikaze tutafika,
fika
she is calling
mungu akamsikia, akavumilia yote
maana hata mkosaji daima hakosi vyote
akihitimu primary secondary na chuo
Kwa kuwa aliamini elimu ndiyo ufunguo
muda ukazidi kwenda akapata kazi nzuri
akachapa kazi akapata pesa na umashuhuri
aliishi vizuri na Watu mtaan kwake
walimuona kama kiongozi Bora Kwa moyo wake
alipoona yatima maumivu alijitonesha
alikumbuka alivyopata tabu kujisomesha
alilipa wema hakuwa mtu wa visa
aliwasamehe mama wa Kambo na baba mzazi
aliwasomesha wadogo zake wapate elimu
akasaidia wazee mahitaji yote muhimu
watoto mnaowatesa ndio watawasaidia
mtoto wa mwenzio ni wako na kiongozi wa Tanzania
(baadae)
She is calling ooh calling
Kwa waliopitia shida aaah
kwani haya maisha, ipo siku yataisha
isha na
usikate tamaa aaah, kwani hata mbuyuu ulianza kama mchichaa
jikaze tutafika,
fika
is calling
ooh calling
Kwa waliopitia shida aaah
kwani haya maisha, ipo siku yataisha
isha na
usikate tamaa aaah, kwani hata mbuyuu ulianza kama mchichaa
jikaze tutafika,
fika
she is calling
instrumental
tongwa records
bin laden
Read Other Latest Song Lyrics Here
Get Fresh updates as they drop via Twitter and Facebook
The post Calling Lyrics by Professor Jay Ft Ali Kiba appeared first on Latest East African & Bongo Flava Music, Songs & Video – Notjustok.
Leave a Reply