Mbwa Mwitu Lyrics by Young Lunya

0
(0)


Mbwa Mwitu Lyrics by Young Lunya

Young Lunya Lyrics

Read and sing aloud Mbwa Mwitu Lyrics by Young Lunya. The song has been well received by fans in Tanzania and beyond.

READ ALSO: Freestyle Session 6 Lyrics by Young Lunya

Read and sing aloud Mbwa Mwitu Lyrics below:

Yeah gang gang mimi nimekuwa
Kwenye mazingira magumu
Ya kigang gang
Sikuweza hata kumantain
Sikuweza hata kufikiria furaha
Maana kila siku ni same pain

Nikimcheki baba kastaafu
Nikicheki mama ana vitenge sijui vitatu
Mdogo wangu anakosa hata viatu
Godoro ni la baba na mama
Wengine tunalalia sakafu
Sasa hapo mimi ilinibidi nijipange maana
Nyumbani kila siku ni ugali tu
Tukila vizuri kande
Labda na tupapa twa kipande
Na mama ni Chips kavu moja
Wote tunaipiga mande

Mambo nikaona yanaenda kuchina
Inafikia muda sister angu anachada mi mwanaume sina
Home nako kukaza fitina
Naonekana kama jibwa koko chafu lililokosa jina
Nikaona siwezi kutukanwa
Bora niingie machakani nitafute cha kufanya
Nitabeba hata magunia ya nyanya

Mateso kaumbiwa mtoto wa kiume
Nikasepa kupambana shida straight up
Nikaingia kwenye makundi
Ambao wananasa ndege kama gundi
Nitawaambia ukweli
Kwa kuiba wana walikuwa mafundi

Ilikuwa ukilizanzisha la kigeto geto
Tunakutimbia na mabeto beto.
Tunaweza tukachukua na kademu kako
Alafu tukakuacha mwenyewe
Na boksi la deto
Ila usiombe tukuibukie na mashine
Jana tulikuwa na mapanga
Ila tuliibuka kivingine

Hata majeshi tunaibuka na mengine
Tunakalisha kuanzia mtaani kwetu
Kuelekea mitaa mingine
Sasa sisi ndo mapanya road
Sisi ndo mambwa mwitu
Na tukipita tunapukutisha kila kitu
Roba za mbao na mambo za kukaba na visu
Na kinanuka wiki mpaka wiki yani kila siku
Alafu sio issue

Ok ganja zipo panga zipo
Sisi tunatimba mahali mkwanja ulipo
Vichwa vimeshapagawa pesa au kifo
Usiombe ukutane na sisi
Danger ka Uviko 19
Mambo yakawa utamu kunoga
Pesa ya wizi hatutumii tena tunakoga
Wanga wakaanza na kuturoga
Ila hawakutuweza muda wote
Tuko nduki na viroba
Tuko nduki na maseke, nduki na machete

Sisi wa kiwalani usiombe
Ukutwe na wa Temeke
Kwanja kama kufyeka tufyeke
Tukishawasili kaa chini au simama tukufanye kiwete
Kisa cha kujiita mbwa mwitu
Kwanza ni wakali kama mbwa
Tuko wengi kama panya
Na hatukabi mtu uchochoroni
Tunakaba barabarani
Na hakuna wanachoweza kutufanya

Picha ni zaidi ya sinema
Picha lilianza hata maduka
Kufungwa mapema
Wananchi wakawa hawana cha kusema
Full kujiamini hata tundu
La sindano tunapenya

Sasa hamna lenye mwanzo
Likakosa kuwa na mwisho
Watu wakatuchoka ila
Walianza na vitisho
Baadae wakawakamata baadhi yetu
Aliyepona hana jicho
Mwenye jicho alichokipata ni kifo

Panya road mbwa zaidi ya fisi
Unyama tuliofanya humsingizii hata Ibilisi
Kikageuka kwa kwetu na sisi
Shida kubwa sana tulipata
Kwa jeshi la polisi
Madifenda yakatimba nane nane
Na wakitimba mabomu ya machozi
Tunashikwa nane nane
Vitambaa usoni tusionane
Virungu vya kwenye mbavu
Ukichekeshwa mbavu zinaweza zisikubane

Hata kama uliachwa unachotwa
Hata kama uliacha
Ndipo tulipogundua tumechokwa
Mpaka hata wazazi waliotupenda
Walianza kutuchoma
Ndipo tulipogundua tumetoswa

Hii stori inafundisha sio kila mwenye kutafuta
Eti ina maana alipoteza
Wengine wanaingia kwenye masuala ya wizi
Kwa sababu wanaamini ndoto zao zilimezwa

Wengine stress za maisha magumu
Wengine wanavurugwa tu na changamoto
Za kuitafuta fedha
Jela sio pazuri kwa vijana
Tukiwekeza kwenye kazi nzuri
Hata kujiajiri tunaweza

Get Fresh updates as they drop via Twitter and Facebook

The post Mbwa Mwitu Lyrics by Young Lunya appeared first on Latest East African & Bongo Flava Music, Songs & Video – Notjustok.

How useful was this post?

Click on a star to rate it!

Average rating 0 / 5. Vote count: 0

No votes so far! Be the first to rate this post.

Be the first to comment

Leave a Reply